LATEST POSTS

Friday, January 3, 2014

Ray C asema hamhurumii Jackie Cliff

 
Jackie Cliff na madawa aliyokamatwa nayo
 Jackie akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya huko China
Jackie cliff kabla hajapatwa na matatizo akiwa katika pozi

ray c

 RAY C

MWANADADA aliyetikisa miaka ya nyuma katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema hana hata chembe ya huruma kwa mwanamitindo Jackie Cliff anayedaiwa kukamatwa na dawa za kulevya huko Macau nchini China, hivi karibuni.
Ray C kupitia akaunti yake ya Instagram, aliandika kuwa, ana hasira sana na watu wanaouza dawa za kulevya kutokana na yeye alipokuwa katika janga hilo alikuwa anakubali kuwapa kila kitu wauzaji ili apate ‘unga’ maana tayari alikuwa ameathirika.
“Omba sana isiwahi kutokea kwa ndugu yako wa karibu, maana mimi nikifikiria mama yangu alivyopata shida wakati mimi naumwa mpaka naambiwa teja, yaani nyie acheni tu, hawa wauzaji wanyongwe kabisa, yaani wao wanafurahia kuona watoto wa wenzao wanaharibika,” aliandika Ray C.
Ray C aliokolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa kumpeleka katika kliniki ya dawa za kulevya Hospitali ya Mwananyamala na kupatiwa matibabu.
Mwanadada huyo alishawahi kutamba na nyimbo zake mbalimbali ikiwemo ‘Chochote Utapata’ ambayo ilifanya vizuri zaidi katika tasnia ya muziki huo.

0 comments: