LATEST POSTS

Sunday, April 13, 2014

Makazi, mazao, barabara zaathirika

 
Wakazi wa kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro wakiwa katika mafuriko kutokana na  mvua zinazonyesha na kusababaisha baadhi ya nyumba kudondoka.

Mvua kubwa zilizonyesha kwa muda wa siku tatu mfululizo mkoani Morogoro, zimeathiri kwa kiwango kikubwa makazi ya watu, miundombinu ya barabara na mazao ya mashambani.
Mvua hizo zilianza Alhamisi mchana na kuendelea hadi jana, zimesababisha watu 400 kukimbia makazi yao na kusimama kwa shughuli za kibiashara katika gulio maarufu la Kikundi mjini Morogoro.
Hali hiyo imetokana na maeneo ya gulio hilo kufurika kwa maji yaliyotokana mvua hizo kiasi cha kuwafanya wafanyabiashara, kufunga biashara zao.
Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wetu katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro, ulishuhudia maji ya mvua hizo yakiwa yamefurika pia kwenye nyumba za watu na kusababisha adha kubwa.
Maeneo ambayo wananchi wake wamekumbwa na mafuriko hayo ni pamoja Msamvu, Mwembesongo, Kihonda, Mafisa, Kichangani na mengine mengi.
Timu hiyo ya waandishi pia ilishuhudia baadhi ya madaraja yakiwa yamefunikwa na maji, makalavati yakiwa yamebomoka na mengine kuziba kwa magogo makubwa na takataka ngumu.
Hali hiyo imesababisha sehemu ya barabara kubomoka
Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, amewahimiza wananchi kuzingatia mipango miji na kuacha kujenga mabondeni.
Alisema kufanya hivyo kitasaidia kutapunguza matukio ya mafuriko yanayosababisha hasara kubwa kwao na kwa Serikali.
Mara kwa mara, Bendera amekuwa akitoa maagizo kwa wananchi kuhama katika maeneo ya mabondeni na kuacha kuendesha shughuli za kilimo jirani na kingo za mito, ili kupuka kusababisha mito kupoteza mwelekeo wa asili na kumwaga maji katika maeneo ya makazi.
Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, amewahimiza wananchi kuzingatia mipango miji na kuacha kujenga mabondeni.
Alisema kufanya hivyo kitasaidia kutapunguza matukio ya mafuriko yanayosababisha hasara kubwa kwao na kwa Serikali.

Mara kwa mara, Bendera amekuwa akitoa maagizo kwa wananchi kuhama katika maeneo ya mabondeni na kuacha kuendesha shughuli za kilimo jirani na kingo za mito, ili kuepuka kusababisha mito kupoteza mwelekeo wa asili na kumwaga maji katika maeneo ya makazi.
Akizungumzia mvua hizo kwa njia ya simu jana, Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo, alisema amewaagiza mkurugenzi na mhandisi wa manispaa kukagua maeneo mbalimbali hasa ya mabondeni ili kujua kiwango halisi cha uharibifu uliotokana na mvua hizo. Habari za awali zilisema zaidi ya watu 400 katika eneo la Mwembesongo, wamelazimika kuhama makazi baada nyumba zao kufurika kwa maji.
Wananchi hao walionekana wakiwa nje ya nyumba zao wakiendelea na jitihada za kuokoa vifaa vya ndani.
Nondo alisema alisema ukaguzi kuhusu mafuriko, utasaidia kujua namna ya kuwasaidia wananchi walioathirika.
Hata hivyo meya huyo alielezea kusikitishwa kwake juu ya baadhi ya wananchi kung’ang’ania kuishi mabondeni licha ya kutakiwa kuondoka.
Alisema halmashauri ilishatoa tahadhari kwab wananchi wanaoishi mabondeni, lakini hawajachukua hatua za kuhama.
“Hata Mamlaka ya Hali ya Hewa ilishatoa tahadhari kwa wanaoishi mabondeni lakini watu wamepuuza,”alisema Nondo.
Pia aliwataka baadhi ya watu kuacha kuzitumia mvua hizo, kuzibua vyoo na mashimo ya maji machafu kama njia ya kuondoa taka maji katika maeneo yao.
Alisema yeyote atakayebainika akifanya hivyo atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kutozwa faini ya Sh 50,000
Baadhi ya walioathirika na mafuriko hayo walisema kuishi kwao katika maeneo hayo kumetokana kukosa maeneo salama waliyoyaomba katika Manispaa ya Morogoro.
Sudi Kipinge ambaye ni mmoja wa waathirika hao, aliiomba serikali kuwapatia mahitaji muhimu kama chakula na magodoro’
Alisema kwa sasa hana chakula na kwamba hiyo imetokana na maji kuingia ndani na kuharibu vyakula.
Kwa upande wake, Maulid Saleh wa Kihonda katika Mtaa wa Kilombero, alisema wakati ananunua kiwanja hakukua na dalili ya kuwa kuna siku mafuriko yataingia.
Alisema mafuriko hayo yametokana na watu kuziba mifereji  hivyo kusababisha eneo hilo kuwa kisiwa.
Mvua hizo zinazotajwa kuwa ni za masika, pia zimesababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara katika Wilaya za Ulanga, Kilosa, Mvomero na Morogoro Vijijini.

0 comments: