LATEST POSTS

Friday, July 11, 2014

Maskini kuku huyu! Jua lake, Mvua yake.

Ni kuku asiyekuwa na manyoya amefumwa na kamera ya mtandao wa Gsengo katika kijiji cha Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Manyoya au magoya kama wengine wanavyoyaita humsitiri kuku katika mvua, kujikinga na baridi kwa kumpa joto, hutumika kama kinga ya kuchomwa na vitu vyenye ncha kali kwani ngozi ya ndege ni laini, hivyo anapoingia kwenye purukushani hususani vichaka vyenye miiba hawezi kudhulika. Sasa anapokuwa katika hali hii ya kukosa magoya ni shida.

0 comments: