Dar es Salaam. Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana
alijikuta akitwishwa masuala mazito kutoka kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya
Usafiri wa Anga (TCAA), ambao walibainisha changamoto nyingi
zinazowarudisha nyuma kutekeleza majukumu yao.
Asilimia kubwa ya changamoto hizo zimesababishwa
na urasimu na migongano iliyopo katika idara za Serikali ambazo kwa
mujibu wafanyakazi hao, zimefanya hadhi ya sekta ya usafiri wa anga
ishuke.
Baadhi ya mambo hayo ni kucheleweshwa kwa rasimu
ya sheria ya usimamizi wa utafutaji na uokoaji katika ajali za ndege
bungeni ambayo haijafanyiwa kazi kwa takriban miaka 10 jambo ambalo
limeifanya TCAA ishindwe kutimiza masharti ya kimataifa.
Mengine ni kuhamishwa kwa mpango mkuu wa usafiri
wa anga nchini (Civil Aviation Master Plan) kwenda kwa Mamlaka ya
Viwanja wa Ndege (TAA) kutoka TCAA kinyume na taratibu za Shirika la
Kimataifa la Usafiri wa Anga (Icao) na upungufu wa mitambo ya kisasa
kusimamia shughuli za anga.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Charles Chacha
alisema mamlaka yake kwa sasa ina changamoto lukuki ukiwemo uhaba wa
wataalamu wa ukaguzi.
0 comments:
Post a Comment