WATU
wawili Rugonzibwa Mujunangoma na Theophillo Bwakea wamefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na
mashitaka ya rushwa baada ya kupokea mgao wa Sh. Milioni 485.1 kutoka
kwenye akaunti ya Tegeta Escrow walizohamishiwa na James Rugemalira.
Katika kesi ya kwanza, aliyekuwa Mwanasheria wa Mamlaka ya Vizazi na
Vifo (Rita) Mujunangoma ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Sheria Wizara
Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi, alisomewa mashitaka yake mbele ya
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Emmilius Mchauru.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai akisaidiana na
Max Ari, ulidaiwa kuwa Februari 5, mwaka 2014 katika benki ya Mkombozi
iliyopo Ilala jijini, mshtakiwa akiwa Mkuu wa Sheria wa wizara hiyo,
alipokea rushwa.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alipokea rushwa ya Sh. Milioni 323.4 kama zawadi kupitia akaunti yake namba 00120102062001 kutoka kwa Mshauri binafsi wa kimataifa na Mkurugenzi wa zamani wa IPTL,James Rugemalira baada ya kuwa mjumbe katika menejimenti ya Rita wakati wa machakato wa kuipitisha IPTL kuiuzia Tanesco umeme.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alipokea rushwa ya Sh. Milioni 323.4 kama zawadi kupitia akaunti yake namba 00120102062001 kutoka kwa Mshauri binafsi wa kimataifa na Mkurugenzi wa zamani wa IPTL,James Rugemalira baada ya kuwa mjumbe katika menejimenti ya Rita wakati wa machakato wa kuipitisha IPTL kuiuzia Tanesco umeme.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alipokea zawadi hiyo kama ofisa wa muda wa kushughulikia masuala ya IPTL.
Mshtakiwa alikana mashitaka yake.
Mshtakiwa alikana mashitaka yake.
Swai alidai kuwa upande wa Jamhuri hauna pingamizi la dhamana na
kwamba mahakama ijielekeze katika hati ya mashitaka fedha anazodaiwa
kuchota mshtakiwa.
Hakimu Mchauru alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa
kujidhamini kwa Sh. Milioni 160 taslimu au hati ya mali isiyohamishika
yenye thamani hiyo ya fedha.
Pia wadhamini wawili wanaofanyakazi serikalini watakaosaini hati ya
dhamana ya Sh. Milioni 10 na mshtakiwa asitoke nje ya Dar es Salaam,
bila kibali cha mahakama.
Mshtakiwa alitimiza baadh ya masharti ya dhamana ambapo hakimu
alisema mahakama imempa dhamana ya muda hadi Januari 16, mwaka huu hati
za mali zake zitakapohakikiwa.
Katika kesi ya pili, aliyekuwa mjumbe wa kitengo cha kuidhinisha
Tanesco kununua umeme wa IPTL, Wizara ya Nishati na Madini, Injinia
Bwakea kwa sasa mtumishi wa Wakala wa Umeme Vijijini(REA), alisomewa
mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi.
Swai alidai kuwa Februari 12, mwaka 2014 mshtakiwa akiwa Injia Mkuu
wa REA, alipokea rushwa ya Sh. Milioni 161.7 kupitia akaunti namba
00410102643901 ya Tegeta Escrow kama zawadi kutoka kwa Mkurugenzi
Rugemalira.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alipokea zawadi hiyo baada ya kuwa mjumbe
aliyeandaa sera zinazohusu sekta binafsi kuzalisha na kuuza umeme kwa
Tanesco.
Mshtakiwa alikana mashitaka yake.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana na kwamba upelelezi umekamilika.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana na kwamba upelelezi umekamilika.
Hakimu Moshi alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka
serikalini au wanaofanyakazi katika taasisi zinazotambulika watakaosaini
hati ya dhamana ya Sh. Milioni 20 kila mmoja.
Pia alisema mshtakiwa asitoke nje ya Dar es Salaam, bila kibali cha mahakama.
Mshtakiwa alitimiza masharti ya dhamana na kesi yake itatajwa Januari 26, mwaka huu.
Mshtakiwa alitimiza masharti ya dhamana na kesi yake itatajwa Januari 26, mwaka huu.
Jana saa 2:00 asubuhi katika viunga vya mahakama ya Kisutu, watumishi
na watu mbalimbali waliingia katika eneo hilo huku kukiwa na minong’ono
kwamba wanaotuhumiwa ufisadi wa Escrow watafikishwa mahakamani hapo.
Pia waandishi wa habari waligawanyika katika makundi tofauti huku
wakijadili na kutafatuta wadau wao kujua kuhusu ujio wa watuhumiwa hao.
Mapema jana saa 5:42 asubuhi vigogo hao walitinga mahakamani hapo na kwenda kusomewa mashitaka yao yanayowakabili.
0 comments:
Post a Comment