JANA usiku ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliwaaga kwa
huzuni wasanii katika tasnia mbalimbali nchini na kuwaahidi kuendelea
kuwa mlezi wao baada ya kumaliza muda wa kuongoza nchi siku 90 zijazo.
Usiku huo uliokuwa maalum kumuaga Rais Kikwete na kumkaribisha
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli uliambatana na burudani na
chakula cha usiku kwa pamoja.
Moja ya mambo aliyoyazungumza Rais Kikwete ni kuwasaidia wasanii
katika kazi zao za sanaa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananufaika
kupitia kazi zao.
“Nchini Marekani kuna msanii wa kike anaitwa Tylor Swift ambaye
alifanikiwa kutoka kimuziki na kwa mwaka wa kwanza alilipwa zaidi ya
dola milioni 40 kwa kazi zake za muziki. Akawa ana uwezo wa kumpata
mwanaume yeyote. Kuna kipindi alikuwa na mmoja wa wanaounda Kundi la One
Direction yote hiyo ni kufanikiwa kwa kazi zake.
“Leo hii wasanii wetu wanafanya kazi kubwa ya kurekodi, kutunga
nyimbo na script lakini mwishoni kazi yake anamkabidhi mtu kwa malipo
kiduchu na pesa nyingi anapata mwingine.
“Niwapongeze nimeshakaa na nyinyi vikao vingi kuhusiana na sanaa,
nimesaidia kufunguliwa kwa studio ya kurekodia. Nikki wa Pili ameongea
kuhusiana na kulipwa malipo kiduchu kutokana na miito ya simu. Utasikia
kama unapenda wimbo huu bonyeza nyota! Msanii anapata hela ndogo wao
wanatengeneza nyingi. Hilo nalifanyia kazi lipo Cosota kwa sasa.
“Najua hata kama nikimaliza muda wangu bado nitaendelea kuwa mlezi wenu kwa sababu nitakuwa mtu maarufu,” alisema Kikwete.
Katika hafla hiyo, wasanii walipata fursa ya kupiga picha (selfie) na
Rais Kikwete sambamba na kucheza naye nyimbo mbalimbali za zamani za
DDC zilizopigwa na msanii kutoka THT, Alice pamoja na Shakira.
Hafla hiyo ilifana pia pale alipopanda Dkt. John Magufuli na kwenda
kwenye eneo la kupigia ngoma akiambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya
CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambapo naye alichukuwa gitaa
na kuanza kutoa burudani kwa wasanii.
0 comments:
Post a Comment