LATEST POSTS

Friday, December 20, 2013

RAIS KIKWETE ATENGUA UTEUZI WA MAWAZIRI WANNE

Kufuatia sakata la ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na Watendaji wakati wakitekeleza zoezi la operation tokomeza majangili, Rais Jakaya Kikwete amelazimika kutengua uteuzi wa Mawaziri wanne akiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Kagesheki.

Wabunge waliongea kwa uchungu na hisia kali bungeni leo wakati wakitoa michango yao baada ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira chini ya Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Lembeli kuwasilisha taarifa yao ambao imetokana na uchunguzi waliofanya katika maeneo kulikofanyika matukio hayo.

Wabunge wote bila kujali itikadi zao, waliungana kwa pamoja na kusisitiza kwamba, vitendo walivyofanyiwa Watanzania wenzetu havikuwa vya kiustaarabu, ni vya unyanyasaji wa hali ya juu na ni vya kiukwaji wa Haki za Binadamu hivyo wote waliohusika katika unyanyasaji huo wachukuliwe hatua za kisheria. Na kwa upande wa Mawaziri ambao Wizara zao zimetajwa kuhusika katika utekelezaji wa zoezi hilo nao wajiuzulu ili kurudisha imani kwa Wananchi.
Baada ya michango hiyo ya Wabunge, Mhe.Balozi Kagasheki alisimama na kutangaza kujiuzulu.
 
 Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Sued Kagasheki.

 
 Mhe. Lisu ni mmoja kati ya Wabunge waliochangia michango ya nguvu kuhusiana na kilichojitokeza katika operation ya tokomeza ujangili
http://www.ibn-tv.com/wp-content/uploads/2012/08/KILONGO.jpg
 Mhe. Anne Kalango Malecela naye alichangia kwa nguvu zote

 
Mhe. Lema naye hakubaki nyuma.  

Sambamba na Balozi Kagesheki, wapo mawaziri wengine watatu akiwemo Waziri wa Maendeleo ya mifugo Dk. Mathayo David.

0 comments: