LATEST POSTS

Wednesday, September 11, 2013

WAHESHIMIWA MADIWANI WA HALMASHAURI YA KALIUA WAFANYA ZIARA YA KUJIFUNZA JIJINI MWANZA

Jopo la Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri mpya ya Wilaya ya Kaliua wafanya ziara ya kujifunza katika jiji la Mwanza. Waheshimiwa hao ambao waliambatana na Wataalamu watano wa Halmashauri hiyo, walitembelea kiwanda cha bia TBL Mwanza, Hifadhi ya wanyama ya Serengeti na Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Hebu safiri nami katika ziara hii kwa njia ya picha kwani nami nilikuwepo katika msafara huo.

Hapa msafara ukiwa katika kiwanda cha bia cha TBL cha mjini Mwanza. Hapa Waheshimiwa Madiwani walipata fursa ya kujionea hatua mbalimbali za utengenezaji wa bia kuanzia hatua ya mwanzo hadi ya mwisho.

                          Usafiri huu ndio uliotumika kututembeza katika sehemu zote tulizozitembelea.
Msafara ukiingia kiwandani
                                    
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mhe.John Kadutu (J.K) mwenyeshati la maua maua pamoja na Waheshimiwa wenzake wakipata maelezo kutoka kwa Mwenyeji wao
Hii ni shayiri mojawapo ya malighafi muhimu inayotumika kutengeneza bia. Zao hili liliwavutia sana Waheshimiwa madiwani wa Kaliua na wakatamani sana wakalilime Wilayani kwao lakini pozi liliwaishi mara baada ya kuelezwa kuwa, zao hili la Shayiri linastawi ama linalimwa katika maeneo yenye baridi kama vile Mbeya na Kilimanjaro.


Hiki ni kifaa ambacho hutumika kuchujia bia ili kuondoa makapi makapi katika bia.

0 comments: