Shirika moja la kutetea haki za wanawake mjini
Naiorbi Kenya, Covaw,linataka Gavana wa Nairobi Evans Kidero akamatwe
mara moja na kushitakiwa kwa kosa la kumzaba kofi mwanasiaaa mwanamke
ambaye pia ni mwakilishi wa wanawake Bi Rachel Shebesh.
Shirika hilo linasema kuwa linalaani kabisa
dhuluma za kijinsia na kwamba watuhumiwa wa vitendo vya dhuluma dhidi ya
wanawake wanapaswa kufikishwa mahakamani.
Mwaka jana Kidero alimzaba kofi mwakilishi wa maswala ya wanawake wa jimbo la Nairobi Bi Rachel Shebesh.
Purukushani lilizuka baada ya Bi Shebesh ambaye
ni mwanasiasa mashuhuri mjini Nairobi kwenda katika ofisi ya Kidero
akiwa ameambatana na wafanyakazi wa baraza la jiji waliokuwa wanagoma
wakidai nyongeza ya mishahara.
Gavana Kidero naye alikuwa amerejea kutoka
kwenye mkutano na Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, alipokutana ana kwa
ana na Shebesh na baadhi ya wafanyakazi wa baraza la jiji.
Hapo ndipo kukazuka sokomoko huku Kidezo akimzaba kofi Bi Shebesh mbele ya watu waliokuwa wameambatana nao.
Baada ya tukio hilo wanasisa hao waliandikisha taarifa kwa polisi huku Kidero akimlaumu Shebesh kwa kumshambulia.
Jumatatu, mahakama kuu ilimzuia mwendesha
mashitaka mkuu Keriako Tobiko kumfungulia mashitaka Gavana Kidero, saa
chache baada ya jaji katika mahakama hiyo kumruhusu Shebesh kumfungulia
mashitaka Gavana Kidero.
Wanasiasa hao wawili walikosa kutatua kesi yao
nje ya mahakama huku wakili wa Shebesh akisema kuwa mteja wake amesubiri
bila jibu Kidero atimize matakwa yake.
Chanzo: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment