LATEST POSTS

Wednesday, January 15, 2014

Ni kweli Jack Cliff katoka au?

Ubongo wangu umekua mgumu kuiamini habari hii. Na kama ni kweli, imekuaje hadi aachiwe huru. Na je, hali ya warembo hawa wanaokamatwa na madawa ya kulevya, kuwekwa mahabusu kwa kipindi kifupi kisha kuachiwa huru, jamii inajifunza nini katika hili? Jibu unalo mwenyewe mdau wangu. Mimi sina neno tena. Heri nikae kimya nijikaangie dagaa zangu na bamia na ugali nile, ninywe na maji kisha nilale. Eeh! Nifanye nini sasa? Habari ndio hiyo.

Tanzania's Boss Lady


nilianza kuchoka mwenzenu




0 comments: